WITO WA USAILI – MAFUNZO YA MADEREVA WANAWAKE

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini – LATRA kwa kushirikiana na Benki ya Dunia  ilitangaza nafasi za ufadhili wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madereva wanawake ili kukidhi sifa za kuendesha magari yote ya abiria.

Mamlaka inawataarifu waombaji 231 kuhudhuria usaili utakaofanyika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji – NIT, kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam, siku ya Jumatatu tarehe 28 Oktoba, 2019 kuanzia saa moja asubuhi.

Majina ya waombaji wanaoitwa yanapatikana katika tovuti ya LATRA (www.latra.go.tz) na kurasa za mitandao ya kijamii za LATRA.

Waombaji wafike na vyeti au leseni zao halisi (sio nakala) na watajitegemea gharama za usafiri, chakula na malazi. Kwa maelezo zaidi wasiliana na mratibu wa mafunzo kupitia 0713-818-958, 0715-750-100 au barua pepe rector@nit.ac.tz

Imetolewa na;

Mkurugenzi Mkuu,

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

22 Oktoba, 2019 ful Accent 4