TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MATUMIZI YA TIKETI MTANDAO KWENYE MABASI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

             Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

TAARIFA KWA UMMA

 MATUMIZI YA TIKETI MTANDAO KWENYE MABASI

Mamlaka inawaagiza wasafirishaji wote wa abiria kwa mabasi kuzingatia masharti ya leseni za usafirishaji na matakwa ya Kanuni za Leseni za Usafirishaji – Magari ya Abiria zilizotangazwa kwa tangazo na 76 kwenye gazeti la Serikali Februari 7, 2020 kama ifuatavyo; 

 • Kanuni ya 4(2)(c); “Leseni ya kusafirisha abiria itatolewa kwa muombaji aliyesajiliwa kwenye mfumo wa tiketi za kielektroniki ulioidhinishwa na Mamlaka”.
 • Kanuni ya 24(b)(d); “Msafirishaji mwenye leseni ya kusafirisha abiria wa masafa marefu ahakikishe anatoa tiketi za kielektroniki kwa abiria.”

Mamlaka inawataka wasafirishaji watoe tiketi za kielektroniki kama kanuni zinavyoelekeza. Kuanzia tarehe 6 Januari, 2021 hakuna msafirishaji atakayeruhusiwa kusafirisha abiria bila kutoa tiketi za kielekroniki kwa abiria wote katika njia zifuatazo;

 1. Dar-es-Salaam – Tanga
 2. Tanga – Arusha
 3. Dar es Salaam – Lindi
 4. Dar es Salaam – Mtwara
 5. Dar es Salaam- Iringa
 6. Dar es Salaam – Njombe
 7. Dar es Salaam – Ruvuma
 8. Dar es Salaam – Mbeya
 9. Dar-es-Salaam-Tunduma
 10. Dar es Salaam – Rukwa
 11. Dar es Salaam – Morogoro
 12. Dar es Salaam – Kilombero
 13. Dar es Salaam – Ifakara
 14. Dar es Salaam – Malinyi
 15. Dar es Salaam – Mahenge

Maelekezo ya utekelezaji wa agizo hili kwenye njia nyingine yatatolewa hivi karibuni.

Imetolewa na;

Mkurugenzi Mkuu,

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

4 Januari, 2021