KWA WASAFIRISHAJI WOTE

Mamlaka inawakumbusha wasafirishaji wote kuzingatia kanuni ya 40 na 41 ya Kanuni za Leseni za Usafirishaji (Mabasi ya Abiria) za mwaka 2020  zilizotangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na.76 la tarehe 07/02/2020.

Pamoja na mambo mengine, kanuni hizi zinataka mabasi yote ya masafa marefu kutoa huduma zake kwa kuzingatia ratiba zilizotolewa na Mamlaka.

Kutokuzingatia kanuni hizi ni kosa kisheria na adhabu yake itatolewa kwa mujibu wa kifungu cha 42 (i) cha Sheria Na.3 ya Mamlaka ya Udhibiti usafiri Ardhini ya mwaka 2019.

IMETOLEWA NA

MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI