Imewekwa: 12 Nov, 2024
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!- Shukran
- Namshukuru Mwenyezi MUNGU mwingi wa Rehema kwa kuendelea kutupa uhai, afya na kuibariki Serikali yetu ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
- Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
- Mhe. Dotto Mashaka Biteko (Mb), Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
- Mhe. Prof. Makame M. Mbarawa (Mb), Waziri wa Uchukuzi kwa kuendelea kusimamia vizuri Wizara na Taasisi zake.
- Pia nashukuru kwa heshima niliyopewa na LATRA ya kuwa mgeni Rasmi katika hafla hii ya kukabidhi kadi za utambuzi kwa wahudumu wa mabasi ya abiria waliokidhi vigezo baada ya kupata mafunzo, kufaulu na kusajiliwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).