Idara inatekeleza kazi zifuatazo;-
- Kuandaa na kutekeleza mipango ya maendeleo ya rasilimali watu;
- Kusimamia uajiri na kuwapanga wafanyakazi;
- Kusimamia mfumo wa mishahara na taarifa za rasilimali watu;
- Kusimamia mchakato wa tathmini ya utendaji wa wafanyakazi na kufuatilia utekelezaji wa matokeo ya tathmini;
- Kuandaa Makadirio ya Mwaka ya Mishahara ya Wafanyakazi;
- Kutayarisha na kupitia Sheria na Kanuni za Utumishi, Sera, Mipango ya Utumishi na Muundo wa Mshahara;
- Kuandaa maslahi ya wastaafu;
- Kuandaa, kupitia na kuratibu utekelezaji wa Mpango wa kuandaa kiongozi mbadala;
- Kuratibu na kutekeleza masuala mbalimbali mahala pa kazi;
- Kusimamia uhusiano mahala pa kazi na masuala ya kinidhamu;
- Kuratibu Mikutano ya Baraza la Wafanyakazi;
- Kuratibu masuala ya utawala ya Mamlaka;
- Kusimamia mali za Mamlaka;
- Kutayarisha na kupitia Sera, taratibu na miongozo ya utawala;
- Kusimamia huduma za Masijala;
- Kusimamia masuala ya ustawi wa wafanyakazi (fidia, afya, usalama, mazishi); na
- Kuwezesha utoaji wa usalama, usafi wa ofisi, usafiri na huduma za jumla.