Dira
Nchi yenye huduma za Usafiri Ardhini zilizo salama, za uhakika na rafiki kwa mazingira
Dhamira
Kusimamia huduma za Usafiri Ardhini kwa kutoa leseni, kuzifuatilia na kukuza ushindani kwa ajili ya ustawi wa Watanzania
Misingi Mikuu
a) Uweledi
Tunaonesha maarifa, ujuzi na mtazamo chanya kwenye kazi zetu
b) Uwajibikaji
Tunajitahidi kuwajibika kwa matendo yetu;
c) Kufanya kazi kwa pamoja
Tunafanya kazi kwa pamoja ili kufikia malengo yetu tuliyojiwekea;
d) Uadilifu
Tuna uaminifu na uadilifu katika kuwahudumia wadau wetu;
e) Uwazi
Tunatekeleza majukumu yetu kwa uwazi na kwa ushirikiano; na
f) Ubunifu
Tunajitahidi kutafuta njia bora za kuongeza thamani ya huduma zetu.