Kitengo kinafanya kazi zifuatazo;
- Kuandaa na kupitia mikakati/mipango ya mawasiliano;
- Kutoa elimu kwa umma kuhusu shughuli za Mamlaka;
- Kukuza taswira nzuri ya Mamlaka;
- Kusimamia mikutano ya washikadau kuhusu shughuli za Mamlaka;
- Kuratibu malalamiko na maoni yanayopokelewa kutoka kwa majukwaa mbalimbali, kuyawasilisha kwa Kurugenzi/Vitengo husika kwa hatua zinazofaa;
- Kusimamia usambazaji wa taarifa kwa wadau husika (umma, vyombo vya habari)
- Kusimamia itifaki na utaratibu unaohusiana na wageni/ziara rasmi za Mamlaka;
- Kusimamia ushiriki wa vyombo vya habari kwa Mamlaka;
- Kusimamia Tovuti na maudhui ya mitandao ya kijamii ya Mamlaka;
- Kutayarisha hotuba mbalimbali, makala za habari na Machapisho;
- Kusimamia vyombo vya habari vya kielektroni kwa ajili ya Mamlaka; na
- Kusimamia shughuli za hisani kwa jamii