Tunahudumia na kuwajali wadau wetu wote wanaotumia Usafiri wa Barabara pamoja na Usafiri wa Reli. Wadau wa Mamlaka hii ni Wasafirishaji wa mabasi ya njia ndefu na mabasi ya miji na majiji, magari ya mizigo, madereva wa mabasi na malori, watoa huduma wa magari maalumu ya kukodi, watoa huduma wa teksi mtandao, abiria, taasisi za umma pamoja na wananchi kwa jumla