Kazi
Kurugenzi inafanya kazi zifuatazo;
- Kukuza ushindani na kuzuia ukiritimba katika sekta ndogo ya usafiri wa barabarani;
- Kuandaa na kupitia Sheria na Kanuni za huduma za usafiri wa barabara;
- Kutoa msaada kiufundi kwa uandaaji wa taratibu na viwango;
- Kusimamia utoaji wa leseni na/au usajili wa vyombo vya moto kibiashara kwa kuzingatia mahitaji ya udhibiti;
- Kuhakikisha uzingatiaji wa kanuni na viwango kwa vyombo vya moto kibiashara;
- Kuunda na kupitia upya kanuni za maadili kwa watoa huduma na watumiaji wa huduma za usafiri wa barabara kibiashara;
- Kushirikiana na Jeshi la Polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi na Wizara yenye dhamana ya usafiri kwenye masuala yanayohusu usafiri ardhini; na
- Kuratibu huduma za usafiri wa mipakani.