Kitengo kinafanya shughuli zifuatazo:-
- Kuratibu mashauri yaliyo Mahakamani chini ya mwongozo wa ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali;
- Kuratibu vikao vya Bodi chini ya mwongozo wa Katibu wa Bodi;
- Kutoa maoni ya kisheria kwa Mamlaka;
- Kuandaa na kupitia Kanuni chini ya Sheria ya Mamlaka na Sheria za kisekta;
- Kufanya taratibu za marekebisho ya Sheria za Mamlaka;
- Kuwezesha taratibu za mapitio ya maamuzi ya Mamlaka kwa utaratibu wa ndani;
- Kufuatilia uzingatiaji na kutekeleza wa Sheria za Mamlaka;
- Kuiwakilisha Mamlaka katika kesi zilizopo Mahakamani au katika Mabaraza zenye maslahi ya Mamlaka;
- Kutoa uelewa wa kisheria kwa wadau wa Mamlaka; na
- Kutunza Muhuri wa Mamlaka