Idara ya Usimamizi wa Vyombo vya Usafiri wa Reli inatekeleza kazi zifuatazo;: -
- Kusajili na kuwaidhinisha waendeshaji wa treni;
- Kuandaa, kupitia na kufuatilia utekelezaji wa viwango na kanuni za usalama wa vyombo vya usafiri wa reli;
- Kufuatilia utekelezaji wa mifumo ya usimamizi wa usalama wa vyombo vinavyotoa huduma ya usafiri wa reli vinavyomilikiwa na watoa huduma za reli;
- Kutoa ushauri kwa watoa huduma kuhusu vyombo vya usafiri wa reli vinavyofaa;
- Kuchunguza ajali na matukio yanayohusiana na vyombo vya usafiri wa reli;
- Kutoa leseni na vibali vya matumizi ya vyombo vya usafiri wa reli; na
- Kuthibitisha ubora wa usalama wa vyombo vya usafiri wa reli.
- Kuidhinisha matumizi ya vyombo vya usafiri wa reli kabla ya kuanza kutumika.