Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Kurugenzi ya Usalama wa Mazingira

Kzi
Kurugenzi inafanya kazi zifuatazo;-

  • Kuratibu usalama wa usafiri ardhini;
  • Kuongoza juhudi za ulinzi wa mazingira kwenye sekta zinazodhibitiwa;
  • Kusimamia ukaguzi wa lazima wa vyombo vya moto kibiashara na magari ya mizigo;
  • Kutunza rejista ya wasafirishaji, madereva na wahudumu wa vyombo vya usafiri wa umma na magari ya mizigo;
  • Kuandaa miongozo ya mitihani na uthibitishaji wa madereva pamoja na usajili wa wahudumu wa vyombo vya moto kibiashara na magari ya mizigo;
  • Kutoa, kuhuisha na kufuta vyeti vya madereva na wahudumu wa vyombo vya moto kibiashara vilivyoidhinishwa na Mamlaka; na
  • Kuwasiliana na wadau likiwemo Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Jeshi la Polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara yenye dhamana ya uchukuzi na wadhibiti wengine kuhusu masuala ya usalama na mazingira.
Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo