Idara inatekeleza kazi zifuatazo;
- Kuandaa na kupitia viwango vya usalama na mazingira katika usafiri wa barabara;
- Kufuatilia utekelezaji wa viwango vya usalama barabarani na mazingira;
- Kufanya ukaguzi wa lazima kwa magari ya kibiashara;
- Kuandaa na Kuratibu utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa usalama wa ardhini;
- Kuanzisha, kukagua na kufuatilia utendaji kazi wa mifumo ya usalama usafiri ardhini (yaani, Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari); na
- Kuchunguza ajali za barabarani na kusambaza matokeo