Idara ya Umeme, Ishara na Mawasiliano inatekeleza kazi zifuatazo;: -
- Kutayarisha, kupitia na kufuatilia utekelezaji wa viwango na kanuni za usalama wa umeme ishara na mawasiliano ya reli;
- Kufuatilia utekelezaji wa Mifumo ya Usimamizi wa Usalama wa Umeme, Ishara na mawasiliano katika uendeshaji wa treni;
- Kufuatilia utendajikazi wa mifumo ya umeme, Ishara na mawasiliano kwenye uendeshaji wa treni;
- Kuchunguza ajali na matukio yanayohusiana na hitilafu za umeme, ishara na mawasiliano; na
- Kuthibitisha ubora wa mifumo ya umeme, ishara na mawasiliano katika uendeshaji wa Treni.
- Kuidhinisha mifumo ya umeme, ishara na mawasiliano kabla ya kuanza kutoa huduma za usafirishaji wa treni.