Kazi
Kurugenzi inafanya kazi zifuatazo;
- Kukuza ushindani na kuzuia ukiritimba katika sekta ndogo ya reli;
- Kutoa, kuhuisha na kufuta vibali na leseni za uendeshaji usafiri wa reli;
- Kuandaa, kupitia na kufuatilia, viwango na kanuni za usalama wa reli;
- Kuandaa kanuni za maadili kwa watoa huduma wa sekta ndogo ya reli.
- Kusajili na kuthibitisha wahudumu (dereva na gadi) katika uendeshaji wa treni;
- Kuidhinisha matumizi ya miundombinu ya reli, mifumo ya usalama na vipengele visivyo vya kawaida vinavyohusiana na usalama wa vyombo vya usafiri kwenye reli;
- Kutathmini na kutoa ushauri wa maboresho ya utendaji wa sekta ndogo ya reli;
- Kuthibitisha ubora wa vitendea kazi na miundombinu ya reli;
- Kuchunguza vyanzo vya ajali na matukio hatarishi ya kiusalama kwenye miundombinu ya reli, vyombo vya usafiri pamoja na mazingira; na
- Kukuza ushirikiano na nyanja nyingine za usafiri (kama vile barabara).