Idara inatekeleza kazi zifuatazo;
- Kutoa, kuhuisha na kufuta cheti kilichoidhinishwa na Mamlaka kwa madereva;
- Kutoa, kuhuisha na kufuta kadi ya usajili kwa wahudumu wa vyombo vya moto kibiashara;
- Kutoa kibali cha taaluma ya udereva kwa madereva wanaovuka mipaka;
- Kuanzisha na kusimamia vituo vya kutahini madereva;
- Kuandaa viwango na kuratibu utahini wa madereva;
- Kuandaa na kuhifadhi kanzidata ya madereva na wahudumu wa vyombo vya moto kibiashara