Idara inatekeleza kazi zifuatazo;
- Kuratibu utekelezaji wa masharti ya leseni ya magari ya kibiashara;
- Kuratibu utekelezaji wa masharti ya usajili wa madereva na wahudumu wa vyombo vya moto kibiashara;
- Kuruhusu utoaji wa vikwazo kwa wanaokiuka masharti ya leseni;
- Kushughulikia malalamiko ya wateja yanayohusiana na huduma za magari ya kibiashara;
- Kusimamia ufuatiliaji wa mawakala walioidhinishwa (yaani watoa huduma wa Tiketi za kielektroni wa VTS);
- Kusimamia maagizo yanayotolewa na Mamlaka; na
- Kusimamia kumbukumbu za ufuatiliaji