Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

IDARA YA USHINDANI NA TOZO

Idara inatekeleza kazi zifuatazo;:-

  • Kutathmini na kupendekeza tozo, viwango na malipo mengine kwa huduma za usafiri ardhini;
  • Kufanya tafiti za mara kwa mara za masoko, tathmini na ulinganishaji wa tozo za huduma zinazodhibitiwa kwa ajili ya kuwianisha, utekelezaji wa kanuni za tozo/viwango, kanzidata na usambazaji;
  • Kutathmini ushindani wa tozo zinazotozwa katika ukuaji wa sekta na uwezo wa kuzimudu kwa watumiaji;
  • Kufuatilia matumizi mabaya ya nafasi katika soko ya watoa huduma wenye uwezo mkubwa, ukiritimba au aina zingine za tabia ya kuhodhi;
  • Kuandaa na kupitia upya kanuni za tozo, miongozo na viwango;
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu uandaaji wa mipango ya biashara kwa watoa huduma; na
  • Kubuni na kuendesha mifumo ya usimamizi wa data kuhusu taarifa zilizokusanywa kutoka kwa sekta ndogo inayodhibitiwa
Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo