Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwakutujaalia uzima, afya na fursa ya kuweza kukutana hapa leo ili kupokea
mapendekezo ya mapitio ya nauli za teksi mtandao kutoka kwa wamiliki/waendeshaji wa mifumo wa teksi hizo (Bolt na Uber), kupokea maoni ya
wamiliki wa teksi hizo, madereva wa teksi mtandao, watumiaji wa huduma hizo (abiria) na wadau wengine na kisha kumpa fursa Mdhibiti wa Huduma hizo (LATRA) kufanya tathmini ya mapendekezo hayo kwa kuzingatia taarifa iliyo wasilishwa na maoni ya wadau.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Pili, natoa shukrani za kipekee kwako binafsi na kwa Ofisi yako kwa ujumla kwa kukubali ombi letu na kujumuika nasi katika shughuli hii muhimu ya kupokea maoni ya wadau wa teksi mtandao kutoka Dar es Salaam kwenda vituo vya nje ya Dar es Salaam, na hata nje ya Tanzania (Afrika Mashariki na Afrika).
Tunafahamu kwamba unayo majukumu mengi, makubwa na muhimu katika ratiba zako, lakini umeweza kutenga muda na kufika hapa ili kutimiza jukumu hili ambalo pia ni la maslahi makubwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Wasafiri toka ndani na nje ya Tanzania wenye kutumia usafiri huu wafikapo Dar es Salaam na Taifa letu kwa ujumla. Hii ni bishara njema kwetu, wadau tuliopo hapa na Watanzania wote kwamba tupo pamoja na Serikali yetu kwenye hili.