Imewekwa: 12 Nov, 2024
Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujaalia afya njema na fursa ya kujumuika hapa leo kwa lengo la kuandika historia mpya katika Nchi yetu ya kuwatambua rasmi wahudumu wa mabasi kwa kuwapatia kadi za utambulisho wa wahudumu wa vyombo vya usafiri ardhini waliotimiza vigezo.
Inapendeza sana kuwaona wadau wetu mmefika hapa, hususan wale waliotupa sababu ya kukutana mahali hapa leo ambao ni wahudumu wa vyombo vya usafiri ardhini.