Imewekwa: 23 Dec, 2024
Wakati LATRA inaendelea kutekeleza majukumu yake ya udhibiti, imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali zinazopelekea uhitaji wa kuwa na Kanuni hizi ili kutatua changamoto hizo. Miongoni mwa changamoto ni:
- kutokuwepo kwa Kanuni mahsusi za kushughulikia utoaji, usitishwaji na ufutwaji wa leseni kwa watoa huduma kwa njia ya Reli;
- kutokuwepo kwa Kanuni mahsusi zinazoainisha utaratibu wa kutoa vibali na leseni kwa ajili ya usimikaji na uendeshaji wa usafiri wa waya; na
- kutokuwepo kwa Kanuni mahsusi zinazotoa utaratibu kuhusiana na leseni maalumu kwa ajili ya kutoa huduma za usafiri wa umma