Imewekwa: 21 Feb, 2023
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inautaarifu umma kuwa imesitisha leseni za usafirishaji abiria kwa mabasi 22 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Februari, 2023.
Hatua hii ni kutokana na vitendo vya kuingilia Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS) na kusababisha mfumo kutotuma taarifa ama kutuma taarifa kwa kurukaruka (skipping). Hapa kuna baadhi ya mabasi ambayo baada ya wataalamu wa Mamlaka kufanya uchunguzi, waligundua betri za vifaa vya kufuatilia mwenendo wa mabasi (VTDs) zimeharibiwa na mfumo wa umeme kubadilishwa.