Imewekwa: 20 Sep, 2022
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inautangazia Umma kuwa Makao Makuu yake yatahamia Dodoma kuanzia Jumatatu tarehe 26 Septemba, 2022. Hatua hii ni utekelezaji wa Agizo la Serikali kwa Wizara na Taasisi zake kuhamia Makao Makuu ya Nchi Dodoma.