Imewekwa: 30 Jan, 2026
Kanuni za Tiketi Mtandao za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za mwaka 2024, zilizotangazwa na Serikali (Tangazo la Serikali Na. 23 la tarehe 12 Januari, 2024), zinaweka sharti kwamba mifumo yote ya Tiketi Mtandao inapaswa kujaribiwa, kuidhinishwa, na mmiliki wake kupata kibali cha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ili itumike rasmi kutoa huduma kwa vyombo vya usafiri wa umma.

