Imewekwa: 05 May, 2025
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inautangazia Umma kuhusu minada ya hadhara itakayofanyika kwa siku tatu; tarehe 20, 23, na 27 Mei, 2025. Lengo la minada hiyo ni kuuza vifaa chakavu vya TEHAMA, Vifaa na Samani za Ofisi. Minada hiyo itafanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mara, Songwe, Mbeya, Lindi, Iringa, Njombe, Pwani, Manyara, Tanga, Singida, Simiyu, Shinyanga, Kilimanjaro, Arusha, Mtwara, Ruvuma, Dodoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Geita, na Mwanza, kama inavyooneshwa katika majedwali yafuatayo: