Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Mkurugenzi Mkuu atoa Pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara
Imewekwa: 20 Sep, 2022

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habibu Suluo, ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Charles Makongoro Nyerere kufuatia vifo vya watu 11 na majeruhi 19 vilivyotokana na ajali mbili mbaya zilizotokea tarehe 19 Septemba, 2022 katika Kijiji cha Chekanao Kata ya Kiperesia Wilayani Kiteto na eneo la Logia Kata ya Sigino Wilayani Babati lenye kona na mteremko mkali, mkoani humo.

Ajali ya kwanza imetokea kwa basi dogo aina ya Mitsubishi lenye namba ya usajili T266 APM lililokua katika mwendo kasi na kusababisha dereva kushindwa kulimudu na kupinduka. Ajali ya pili imetokea kwa gari aina ya Toyota LandCruiser Pickup mali ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lenye namba ya usajili SU37817 kugongana na gari lenye namba ya usajili E7327 aina ya Howo ikiwa na tera namba T2152A la nchini Burundi baada ya breki za roli hilo kufeli.

Soma zaidi

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo