Imewekwa: 05 Feb, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA Habibu Suluo, ametoa salamu za pole kwa Mhe. Omary Tebweta Mgumba, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, kufuatia vifo vya watu 17 na majeruhi 12 vilivyotokana na ajali iliyotokea Ijumaa, tarehe 3 Februari, 2023 saa 4:22 usiku eneo la Magila Gereza, tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe mkoani Tanga.