Imewekwa: 06 May, 2024
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, inasikitika kutangaza kuwa, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mikoa ya Kusini – Mashariki mwa Tanzania, kumekuwa na uharibifu mkubwa wa barabara inayotoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Lindi na Mtwara kupitia Kilwa, katika maeneo ya Somanga, Njia nne, Masaninga, Cheketu na Matandu, ambapo barabara hiyo kwa sasa haipitiki kabisa.