Imewekwa: 10 Jun, 2024
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inawatangazia taarifa ya maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini kuhusu nauli za abiria wa daraja la kawaida kwa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora. Nauli hizi ni baada ya kufanyia kazi maombi yaliyoletwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) na taarifa zilizopokelewa kutoka TRC na wadau wengine.