Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Tuzo za Watoa Huduma Bora za Usafiri Ardhini 2025
Imewekwa: 12 Nov, 2025

Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(a) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Sura ya 413, LATRA ina jukumu la kuhamasisha ushindani wenye ufanisi miongoni mwa watoa huduma zinazodhibitiwa. Katika kutekeleza hilo, pamoja na majukumu mengine, LATRA imekuwa ikitoa tuzo kwa watoa huduma bora za Usafiri Ardhini. Kwa mara ya mwisho, LATRA ilitoa tuzo kwa watoa huduma bora na salama mwaka 2024, katika wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, iliyofanyika Dodoma, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Lengo la tuzo hizo ni kuboresha mazingira ya ushindani wenye tija na ufanisi miongoni mwa watoa huduma, kuchochea uwepo wa mifumo imara na endelevu katika utoaji na upatikanaji wa huduma bora za usafiri ardhini kwa umma kwa kuzingatia Shabaha za Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs 2030). SDGs 2030 inahamasisha uwepo wa huduma za Usafiri wa umma ulio Salama, Unaopatikana, Endelevu, wa gharama nafuu, Unaozingatia mahitaji ya makundi maalum, huduma bora kwa wateja, Ubunifu na Matumizi ya teknolojia.

Soma zaidi

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo