Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Udhibiti wa Usalama kwa Madereva na Wamiliki wa Vyombo vya Moto Kibiashara
Imewekwa: 30 Apr, 2023

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani na wadau wengine, tunaendelea kutekeleza jukumu la kusimamia usalama wa huduma za usafiri kwa magari ya abiria na mizigo nchini kwa mujibu wa Sheria.

Miongoni mwa majukumu yanayotekelezwa na LATRA kwa lengo la kuimarisha usalama ni kuthibitisha madereva na kusajili wahudumu wa vyombo vinavyodhibitiwa. Tarehe 22 Februari, 2023, kwenye kikao cha wadau wa usafirishaji, Mhe. Eng. Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alitangaza kuwa madereva wote wa vyombo vya moto kibiashara wahakikishe wamesajiliwa LATRA kabla ya tarehe 30 Aprili, 2023.

Pakua taarifa kamili

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo