Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

LATRA Logo

Utekelezaji wa Agizo la Serikali - Baadhi ya Mabasi ya Masafa Marefu kuanza Safari Saa 11:00 Alfajiri
Imewekwa: 15 Jan, 2023

Tarehe 16 Disemba, 2022, Mhe. Jumanne A. Sagini (Mb), Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alitoa ridhaa kwa baadhi ya mabasi ya masafa marefu kuanza safari saa 11.00 alfajiri. Utekelezaji wa ridhaa hiyo uliambatana na masharti mbalimbali likiwemo sharti la madereva wa magari yatakayopewa ratiba hizo kuwa wamethibitishwa na kusajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, Sura ya 413 ili kurahisisha ufuatiliaji wa madereva na udhibiti wa ajali zinazosababishwa na makosa ya kibinadamu. Ridhaa hii ya Serikali ilipokelewa vizuri na wamiliki pamoja na madereva wa mabasi ya masafa marefu.

Pakua taarifa kamili

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo