18 Dec, 2025
03:00 Asubuhi
Chuo cha Utalii, Dar es Salaam
Tunawataarifu wadau wote wa sekta ya usafiri ardhini nchini kuwa, Mkutano wa Wadau kwa ajili ya kupokea maoni kuhusu mapendekezo ya kutengeneza Kanuni za Usimamizi wa Madhara ya Uchovu kwa Madereva za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka 2025 uliopangwa kufanyika tarehe 22 Desemba, 2025 umesogezwa mbele hadi tarehe 8 Januari, 2026.
Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Utalii, kilichopo Mtaa wa Shaaban Robert, Jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu kamili asubuhi. Tangazo hili linafuta taarifa ya mkutano wa awali iliyotolewa tarehe 9 Desemba 2025 kupitia gazeti la Mwananchi Namba 9249.

