16 Dec, 2022
3:00 asubuhi
Ukumbi wa Anatouglou
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imepokea maombi kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhusu nauli za abiria kwa treni ya njia ya Reli ya Kisasa – ‘Standard Gauge Railway’ (SGR) zitakavyotumika kwa huduma ya usafiri wa treni za abiria.
Kwa mujibu wa Kifungu Na. 21 cha Sheria Na. 3 ya LATRA, 2019 Mamlaka inapaswa kukusanya maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridhia viwango vya nauli kwa huduma zinazodhibitiwa na Mamlaka ikiwemo nauli za treni.