29 May, 2024
3:00 asubuhi
Ukumbi wa Mikutano wa Arnaoutouglou
Wizara ya Uchukuzi kwa mujibu wa kifungu cha 45 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413 inawaalika wadau wote wa usafiri ardhini kuhudhuria mkutano wa kupokea maoni kuhusu mapendekezo ya maboresho ya Sheria na baadhi ya Kanuni za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA). Mkutano utafanyika tarehe 5 Juni, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Arnaoutouglou uliopo Mnazi mmoja, Dar es Salaam kuanzia saa tatu kamili (3:00) asubuhi.