09 May, 2022
09:30 AM - 12:30PM
JNICC
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inawakaribisha wadau wote wa Mabasi Maalum ya Kukodi kwenye kikao cha pamoja kitakachofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC). Katika kikao hicho, washiriki watafahamishwa kuhusu majukumu ya Mamlaka ikiwa ni pamoja na suala la utoaji wa leseni za mabasi hayo. Vilevile, washiriki watapata nafasi ya kutoa maoni yatakayochukuliwa na kufanyiwa kazi na Mamlaka.