Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Kutuma Maombi Mapya ya Leseni za Magari ya Abiria
Imewekwa: 09 May, 2022

Nyaraka zinazohitajika

a) Kadi ya usajili wa gari;

b) Hati ya bima iliyo hai;

c) Hati ya ukaguzi wa gari kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na risiti yake ya malipo.

d) TALA (kwa maombi ya leseni ya huduma ya usafirishaji gari la kubeba watalii)

e) Leseni ya dereva kwa magari ya abiria

Hatua za Kufuata

a) Kupata linki ya mfumo, ingia kwenye tovuti ya Mamlaka www.latra.go.tz, fungua huduma mtandao kisha chagua RRIMS. (Unaweza pia kupata linki ya mfumo moja kwa moja kwa kuandika www.rrims.latra.go.tz )

b) Itafunguka linki ya mfumo wa RRIMS, kisha ingiza baruapepe na nywila yako kwenye sehemu husika,

c) Chagua neno lililoandikwa Maombi ya leseni, bonyeza maombi ya leseni magari ya abiria,

d) Chagua neno Ongeza gari,

e) Jaza na hifadhi taarifa zinazohitajika,  ambatisha nakala za vielelezo vinavyohitajika  kisha, wasilisha maombi hayo kwenye ofisi ya LATRA ulilochagua,

f) Maombi ya leseni yatashughulikiwa ndani ya saa ishirini na nne (24),

g) Msafirishaji utapata ankara ya malipo (Control number)

h) Utalipia kupitia ankara ya malipo (Control number)/namba ya kumbukumbu ya malipo kwa kutumia huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu. (tigopesa, Mpesa,Airtel Money, Halopesa, T-pesa n.k)  benki na mawakala wa benki (NMB, NBC, Azania, nk)

i) Baada ya malipo unaweza kuchapa leseni yako mtandaoni kupitia akaunti yako ya RRIMS.

Zingatia

Hatua za maombi ya leseni, zitafuatwa na waombaji wa leseni wanaohuisha leseni, kubadili njia/huduma/ratiba baada ya mwombaji wa leseni  kuchagua huduma anayohitaji.

Uhai wa Leseni: Mwaka mmoja

Gharama za maombi ya leseni

i) Unapotuma maombi ya leseni gharama yake ni TZS. 10,000/= au Dola 10

ii) Malipo ya ratiba ya safari kwa magari ya masafa marefu (yanayounganisha mkoa na mkoa au nchi na nchi) ni TZS. 10,000/=

Gharama za leseni

a) Leseni za Mabasi ya Abiria (Shule/wanafunzi, taasisi/Wafanyakazi, Daladala, Mabasi ya Mikoani.)

i) Daraja la Kawaida na Daraja la Kati la Chini

  • Gari linalobeba abiria wasiozidi 15  TZS. 35,000/= au Dola 50
  • Gari linalobeba abiria 15 hadi 25 TZS. 50,000/= au Dola 80
  • Gari linalobeba abiria 25 hadi 45 TZS. 90,000/= au Dola 145
  • ​​​​​​​Gari linalobeba abiria 45 hadi 65 TZS. 100,000/- au Dola 150
  • ​​​​​​​Gari linalobeba abiria zaidi 65 TZS. 140,000/=  au Dola 160

ii) Daraja la Kati la Juu na Daraja la Kifahari

  • Gari linalobeba abiria zaidi ya 25 TZS. 150,000/= au Dola 180

b) Leseni za Magari ya Kubeba Watalii.

  • ​​​​​​​Gari linalobeba abiria wa kitalii wasiozidi 15  ni Dola 50
  • ​​​​​​​Gari linalobeba abiria wa kitalii 15 hadi 25 ni Dola 80
  • ​​​​​​​Gari linalobeba abiria wa kitalii 25 hadi 45 ni Dola 145
  • ​​​​​​​Gari linalobeba abiria wa kitalii 45 hadi 65 ni Dola 150
  • ​​​​​​​Gari linalobeba abiria wa kitalii zaidi 65 ni Dola 160

Zingatia

i)  Ada katika Dola italipwa sawia katika shilingi ya Kitanzania katika siku husika.

ii) Malipo yote yafanyike kwa  ankara ya malipo (Control number)/ namba ya kumbukumbu ya malipo iliyotolewa na Mamlaka.

 

 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo