Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Kutuma Maombi ya Usajili wa Msafirishaji
Imewekwa: 09 May, 2022

Nyaraka zinazohitajika

a) Cheti cha usajili (Kwa Kampuni au Taasisi)

b) Kitambulisho cha NIDA (Kwa mtu binafsi)

Maombi ya kutambuliwa kuwa msafirishaji  yanafanyika kwenye Mfumo wa Usimamizi na Utoaji Leseni za Usafiri wa Barabara na Reli (RRIMS).

Hatua za kufuata

a) Kupata linki ya mfumo, ingia kwenye tovuti ya Mamlaka www.latra.go.tz, fungua huduma mtandao kisha chagua RRIMS. Unaweza pia kupata linki ya mfumo moja kwa moja kwa kuandika https://www.rrims.latra.go.tz

b) Ukiwa katika mfumo, bofya kitufe Jisajili Hapa.

c) Itafunguka linki ya mfumo wa RRIMS kisha ingiza baruapepe na nywila kwenye sehemu husika,

d) Chagua aina ya usajili unaokuhusu, kisha ingiza taarifa zako katika fomu kwa umakini na tuma kwa kubofya kitufe Jisajili. (Kwa mtu binafsi, utatakiwa kuhakiki taarifa zako kwa kutumia namba ya NIDA, kwa Kampuni/Taasisi, utatakiwa kujaza taarifa husika kama zilivyosajiliwa).

e) Baada ya kutuma, ingia kwenye baruapepe uliyojaza, utapata ujumbe utakaokuwezesha kutengeneza na kuthibitisha nywila mpya.

f) Ingia kwenye kwenye mfumo wa RRIMS www.rrims.latra.go.tz kwa kujaza baruapepe na nywila yako.

g) Kamilisha taarifa za Afisa usafirishaji (msimamizi wa magari husika), hifadhi taarifa hizo na wasilisha maombi hayo kwenye tawi la LATRA utakalolichagua,

h) Maombi ya msafirishaji yatashughulikiwa na Maafisa leseni ndani ya saa ishirini na nne (24),

i) Maombi yakishughulikiwa;

  • Kwa mtu binafsi utapata namba ya Cheti cha usafirishaji;
  • Kwa Kampuni/Taasisi utapata ankara ya malipo (control number) ya kulipia.
  • Ankara hii utaipata katika sehemu maalum ya kuangalia Bili.
  • Baada ya kulipa utapata cheti cha Usafirishaji ambacho utachukua katika ofisi ya Mamlaka iliyopo karibu.

j) Baada ya maombi ya msafirishaji kufanyiwa kazi, akaunti yako ya mfumo itakuwa tayari na utaweza kuendelea kufanya maombi mengine kulingana na mahitaji yako.

Gharama

a) Bure (Kwa mtu binafsi)

b) Malipo ya cheti cha Usafirishaji TZS.100,000/= (Kwa kampuni/ Taasisi) Malipo hufanyika kwa mara moja tu kwa muda wote wa kutoa huduma kama msafirishaji.

 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo