Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Kujisajili kwenye Mfumo wa RRIMS
Imewekwa: 12 May, 2023

Nyaraka zinazohitajika

a. Cheti cha usajili (Kwa Kampuni au Taasisi) –

b. Kitambulisho cha NIDA (Kwa mtu binafsi)

Hatua za Kufuata

Ili kujisajili kwenye mfumo, fungua akaunti kupitia anwani ya www.rrims.latra.go.tz

a)  Kwa mtu binafisi (Tumia namba ya kitambulisho cha NIDA),

b) Kwa Kampuni au Taasisi (Tumia namba ya cheti cha usajili wa kampuni au taasisi)

c) Kwa mtu binafsi unayetumia namba ya kitambulisho cha NIDA, utatakiwa kuthibitisha taarifa zako kwa kujibu kwa usahihi maswali walau matatu yanayohusiana na taarifa zako kutoka NIDA. Kwa Kampuni/Taasisi, jaza taarifa husika kama zilivyosajiliwa na BRELA au Mamlaka iliyosajili Taasisi husika)

Jinsi ya kuingia kwenye Mfumo  wa RRIMS

a) Ingia kwenye tovuti ya Mamlaka www.latra.go.tz, fungua huduma mtandao kisha chagua RRIMS kupata linki ya mfumo. Unaweza pia kupata linki ya mfumo moja kwa moja kwa kuandika https://www.rrims.latra.go.tz

b) Ukiwa katika mfumo, chagua sehemu iliyoandikwa Jisajili Hapa

c) Chagua aina ya usajili (mtu binafsi/Kampuni/Taasisi), kisha jaza taarifa zako kwa umakini na zitume kwa kuchagua sehemu iliyoandikwa Jisajili.

d) Baada ya kutuma, fungua baruapepe kwa kutumia anwani ya baruapepe uliyojaza, ili kupata ujumbe utakaokuwezesha kutengeneza na kuthibitisha nywila mpya kwa ajili ya matumizi ya mfumo.

e) Kama umesahau nywila, ingia kwenye mfumo https://www.rrims.latra.go.tz, chagua sehemu iliyoandikwa umesahau nywila? na kisha weka baruapepe yako chagua sehemu iliyoandikwa badili, baada ya hapo fungua baruapepe yako  utaona ujumbe wa jinsi ya kubadilisha nywila yako.

Gharama:

a) Kwa mtu binafsi: Bure

b) Kwa Kampuni au Taasisi: TZS. 100,000/=

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo