Nyaraka zinazohitajika
a) Kadi ya usajili wa gari
b) Hati ya bima iliyo hai;
c) Hati ya ukaguzi wa gari kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na risiti yake ya malipo.
Hatua za Kufuata
a) Kupata linki ya mfumo, ingia kwenye tovuti ya Mamlaka www.latra.go.tz, fungua huduma mtandao kisha chagua RRIMS. (Unaweza pia kupata linki ya mfumo moja kwa moja kwa kuandika www.rrims.latra.go.tz )
b) Itafunguka linki ya mfumo wa RRIMS, kisha ingiza baruapepe (na nywila yako kwenye sehemu husika,
c) Chagua neno lililoandikwa Maombi ya leseni, chagua sehemu iliyoandikwa usafiri wa kukodi,
d) Chagua neno Ongeza gari,
e) Jaza na hifadhi taarifa zinazohitajika, ambatisha nakala za vielelezo vinavyohitajika kisha, wasilisha maombi hayo kwenye ofisi ya LATRA uliyochagua,
f) Maombi ya leseni yatashughulikiwa na Maafisa leseni ndani ya saa ishirini na nne (24),
g) Msafirishaji utapata ankara ya malipo (Control number)
h) Utalipia kupitia ankara ya malipo (Control number) kwa kutumia huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu. (tigopesa, Mpesa,Airtel Money, Halopesa, T-pesa n.k) benki na mawakala wa benki (NMB, NBC, Azania, nk)
i)Baada ya malipo unaweza kuchapa leseni yako mtandaoni kupitia akaunti yako ya RRIMS.
Zingatia
Hatua za maombi ya leseni, zitafuatwa na waombaji wa leseni, wanaohuisha leseni, kubadili njia/huduma/ratiba baada ya mwombaji wa leseni kuchagua huduma anayohitaji
Uhai wa Leseni: Mwaka mmoja
Gharama za maombi ya leseni
Unapotuma maombi ya leseni gharama yake TZS. 10,000/= au Dola 10
Gharama za leseni
(i)Leseni za Teksi za Kawaida TZS. 25,000/= au Dola 30
(ii)Leseni ya Teksi za Mtandao TZS.25,000/= au Dola 30
Zingatia
Malipo yote yafanyike kwa ankara ya malipo (control number)/ namba ya kumbukumbu ya malipo inayotolewa na Mamlaka