Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

AGIZO LA MHE. RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN LAWAKUTANISHA BODI YA WAKURUGENZI NA MENEJIMENTI YA LATRA NA TRC
Imewekwa: 02 Feb, 2024
AGIZO LA MHE. RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN LAWAKUTANISHA BODI YA WAKURUGENZI NA MENEJIMENTI YA LATRA NA TRC

Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imefanya ziara katika mradi wa Reli ya kisasa (SGR) na kukagua miundombinu pamoja na mabehewa ya reli hiyo, ziara hiyo imefuatiwa baada ya tamko la Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania ambaye ameagiza mpaka Julai, 2024 huduma ya reli hiyo ianze kutolewa.

Akizungumza katika ziara hiyo Prof. Ahmed Mohamed Ame ameeleza kuwa LATRA inajukumu kubwa la kusimamia reli na miundombinu yake ikiwa ni pamoja na kusimamia ubora wa huduma zinazotolewa na Shirika la Reli nchini (TRC).

“Kilichofanyika ni kitu kikubwa kwa sababu tumeweza kutengeneza mpango kazi na tumezitaka menejimenti zetu mpango kazi uanze kutekelezwa kimoja baada ya kingine kwa muda maalum na hadi kufikia mwezi mei mambo yote tuliyokubaliana yawe yametimia na ikiwezekana huduma zianze hapo hapo na sio lazima kusubiri mpaka mwezi Julai” ameeleza Prof. Ame.

Kwa upande wake Bw. Ally Karama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TRC amesema ugeni wa leo ulikuwa na lengo la kukagua Reli ya kisasa (SGR) kujua imefikia wapi na inaelekea wapi, katika majadiliano hayo wametoa ukomo wa muda mpaka kufika mwezi Mei mwaka huu vifaa vyote na taratibu muhimu za kuwezesha mradi  ziwe zimeshatimia tayari kwa kuanza kazi.

 “Malengo tuliojiwekea kama bodi ni kuhakikisha kwamba mpaka mwezi mei tuwe na uwezo wa kuanza kazi na sio kungoja mpaka siku iliyowekwa na Mhe.Dkt Samia, tunafahamu LATRA kama mamlaka inayodhibiti usafiri wa reli lazima watupe vyeti ili kutuwezesha kuanza kazi na kuweka njia yetu kuwa wazi na tunaamini chochote kikitokea watatupa ushirikiano kama tukifuata taratibu zote kwanzia sasa mpaka tutakapo anza kutoa huduma kwenda Dodoma Bw. Ally Karama ameeleza.

Naye CPA Habibu Suluo Mkurugenzi mkuu wa LATRA ameipongeza bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya TRC kwa kusimamia mradi mkubwa wenye manufaa makubwa kwa nchi na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla lakini pia ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa uwekezaji huo wa kipekee.

“Watanzania watafurahia uwekezaji huu na sisi LATRA jukumu letu ni kuhakikisha usalama na ubora, mpaka sasaivi haya mabehewa tumeshayakagua tumeona yako katika ubora wa kuanza kutumika, njia tumekagua lakini kuna maeneo yanahitaji kumalizika na kuwekewa fensi kwa sababu hii njia lazima iwe na fensi ya kuwezesha sehemu ambayo reli zinapishana na hilo linafanyika na tunatarajia maeneo ambayo hayajakamilika mpaka mwezi wa tano yatakuwa yamekamilika” ameeleza CPA Suluo.

Aidha CPA Suluo ameongeza kuwa Mamlaka inahakikisha ubora wa kiuchumi na ubora wa kiusalama kwaio niwatake wananchi tushirikiane kulinda miundo mbinu hii kwa sababu uwekezaji huu ni mkubwa sana kwahio tunaomba tutunze rasilimali hii na tuwe walinzi.

Naye Bw. Senzige Kisenge Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC akiongelea ziara ya bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya LATRA kuwa wamejipanga na wapo tayari kutekeleza maagizo ya bodi hiyo.

“Ninachoweza kusema ni kwamba maandalizi yanaendelea vizuri mambo mengi ya kiufundi yamekamilika kwa kiasi kikubwa lakini kabla ujaanza kutoa huduma ili kulinda usalama lazima tufanye majaribio mengi sana na saivi tupo katika hatua za kufanya majaribio ya njia yenyewe na mabehewa, tukishamaliza mamlaka itakuja kuthibitisha na kutupa vyeti na ninachoweza kuwaambia ni kwamba maandalizi yapo vizuri tunakwenda vizuri” Bw. Kisenge amefafanua zaidi.

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo