Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

LATRA Logo

KATIBU MKUU (UCHUKUZI) AWAPOKEA LATRA DODOMA
Imewekwa: 27 Sep, 2022
KATIBU MKUU (UCHUKUZI) AWAPOKEA LATRA DODOMA

Na. Salum Pazzy 

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi, Gabriel J. Migire jana Jumatatu tarehe 26 Aprili, 2022 aliwapokea baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) mara baada ya LATRA kutekeleza maelekezo ya Serikali kuhamishia rasmi makao yake makuu jijini Dodoma.

Akiongea na wajumbe wa menejimenti ya LATRA waliofika ofisini kwake jana, Bw. Migire aliwapongeza wafanyakazi na uongozi wa LATRA kwa kuweza kujipanga kufika Dodoma mapema kufuatia maelekezo ya Serikali yalivyotangazwa na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jumatatu Septemba 5, 2022.

‘Tunafahamu kuwa binadamu ni mzito kufanya mabadiliko, huenda baadhi yenu wakawa bado wanaona uzito katika hatua hii ya awali, napenda kuwahakikishia kuwa mtafurahia maisha ya Dodoma kwa kuwa Dodoma sasa ina fursa nyingi na kadri mnavyoishi huku mtazifahamu na kuzifurahia.’ alisema

Aliongeza kuwa, ni muhimu LATRA kuongeza matumizi ya Serikali Mtandao ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu mbalimbali baada ya kuhamia Mako Makuu ya Nchi Dodoma.

Aidha alisema kuwa, ofisi yake iko tayari kutoa ushirikiano iwapo LATRA itakutana na  changamoto zinazoweza kujitokeza katika siku za awali baada ya kuhamia Dodoma.

Kwa upanda wake, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA Habibu Suluo alisema kuwa LATRA ilijipanga kutekeleza maelekezo ya Serikali tangu mapema na kuwa anawakaribisha wadau mbalimbali kufika ofisi za LATRA Makao Makuu zilizopo eneo la Tambukareli barabara ya Jakaya Kikwete jirani na Jengo la Mkandarasi jijini humo.

“Tangu nilipokabidhiwa ofisi tarehe 11 Julai, 2022 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Gabriel Migire, alinipa maelekezo ya Serikali kuhusu kuhamia Dodoma, hivyo nilishirikiana na wenzangu tukafanya maandalizi yaliyotuwezesha kuhamia Dodoma kwa wakati.” alisema

“Tutaendelea kutoa huduma zetu tukiwa Dodoma, natoa shukrani kwa ushirikano tulioupata kwa Wizara kupitia Katibu Mkuu na viongozi wengine,” aliongeza

Aidha CPA Suluo ametoa shukrani kwa uongozi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kuipatia LATRA baadhi ya samani za  ofisini zilizoiwezesha LATRA kuhamia Dodoma kwa urahisi zaidi.

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo