Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

LATRA YA KABIDHI VIFAA VYA VTS KWA JESHI LA POLISI
Imewekwa: 05 Apr, 2023
LATRA YA KABIDHI VIFAA VYA VTS KWA JESHI LA POLISI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA Prof. Ahmed Mohammed Ame, amekabidhi vifaa vya Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS) ikiwemo runinga mbili, komputa mbili pamoja na komputa mpakato mbili kwa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani ili kudhibiti hali ya usalama kwa vyombo vya moto viwapo safarini na kupunguza ajali nchini.

Makabidhiano hayo yamefinyika katika ofisi za LATRA jijini Dar es Salaam Ijumaa Machi 31, 2023.

 Akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria makabidhiano hayo, Prof. Ahmed amesema kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuongeza ushirikiano uliopo kati ya LATRA na Jeshi la Polisi na kudhibiti ajali ambazo hivi karibuni zimekuwa zikijitokeza.

“Lengo letu ni kuongeza ushirikiano zaidi na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani ili kufatilia mwenendo wa mabasi yawapo safarini, kama mtakuwa wafatiliaji wazuri usalama wa barabarani umekuwa si mzuri na hivi karibuni kumetokea ajali nyingi barabarani zinazo gharimu maisha ya watu wengi na kuharibika kwa mali nyingi” amesema Prof. Ahmed

Aidha Prof. Ahmed ameeleza kuwa moja ya faida ya vifaa ambavyo LATRA imewakabidhi Jeshi la Polisi ni pamoja na kuwawezesha kufatilia mwenendo wa magari ya abiria yawapo safarini kupitia mfumo wa VTS.

“Vifaa hivi vitawawezesha Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kufatilia mwenendo wa mabasi barabarani hasa haya mabasi yanayokwenda masafa marefu (mabasi yanayokwenda mikoani na nje ya nchi) ili kupunguza ajali za barabarani nchini” ameeleza Prof. Ahmed

Kwa upande wake CPA Habibu Suluo Mkurugenzi Mkuu LATRA amekemea madereva na wamiliki wa mabasi ambao wamekuwa wakichezea vifaa vya kufuatilia mwenendo wa magari (VTD) hali inayoongeza hatari ya kupata ajali wakiwa safarini, na kusisitiza hatua za kisheria kuchukuliwa.

“Kiukweli mtu anapochezea vifaa hivi vya kufuatilia mwenendo wa magari maana yake anahatarisha kwa makusudi maisha ya watanzania, hivyo tunatoa onyo kwa madereva na wamiliki wa mabasi waache kuchezea mfumo wa VTS ikiwa wakikiuka watachukuliwa hatua za sheria, wapo ambao tumewafungia hadi siku 30” amesema CPA Suluo

Naye mwakilishi wa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani ACP Meloe Buzema ameishukuru LATRA kwa kukabidhi vifaa hivyo ambavyo vitaongeza ufanisi katika udhibiti wa mwenendo wa magari ya abiria nchini.

“kuwepo kwa teknolojia ya mfumo wa VTS kumesaidia kupunguza viwango vya ajali ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Naamini baada ya kupokea vifaa hivii kutakuwa na mabadiliko makubwa katika kudhibiti ajali za barabarani”. Ameeleza ACP Meloe Buzema .

LATRA imekuwa na desturi yakushirikiana na wadau mbalimbali wa Usafiri Ardhini wakiwemo jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani ili kuboresha huduma za Usafiri nchini ikwa ni pamoja na kupunguza ajali,

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo