Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

MHA. KISAKA: USHIRIKISHWAJI WA WADAU NI MUHIMU KATIKA KUANDAA KANUNI
Imewekwa: 18 May, 2023
MHA. KISAKA: USHIRIKISHWAJI WA WADAU NI MUHIMU KATIKA KUANDAA KANUNI

Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Aron Kisaka amesema ushirikishwaji wa wadau ni muhimu katika kuandaa Kanuni za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) za mwaka 2023 ambazo zitachochea ukuaji wa sekta ya usafiri wa ardhini nchini kwa kutengeneza mazingira bora ya utendaji kazi kwa watoa huduma za usafiri wa ardhini.

Mha. Kisaka ameyasema hayo alipofungua Mkutano wa Kupokea Maoni ya Wadau Kuhusu Rasimu za Kanuni Mpya nane (08) za LATRA uliofanyika Mei 17, 2023 katika ukumbi wa Idara ya Maji Mkoani Mwanza, akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) Bw. Gabriel Migire.

Mha. Kisaka amewaambia wadau hao kuwa ushirikishwaji wa wadau katika uandaaji wa kanuni hizo utasaidia upatikanaji wa Kanuni bora na zenye manufaa makubwa katika sekta ya usafiri ardhini.

“Ushirikishwaji ni sehemu muhimu sana katika uandaaji wa Kanuni hizi, mtashirikishwa kwa siku ya leo na baada ya kupokea maoni yenu kanda ya ziwa yatajumuishwa na maoni ambayo yametolewa Kanda nyingine, wataalamu watakaa kupitia maoni yenu wote na kufanya maboresho kutokana na maoni mliyowasilisha,” amesema Mha. Kisaka.

Aidha, Mha. Kisaka ameongeza kuwa lengo la uandaaji wa kanuni hizo ni kumlinda msafirishaji ambae anatoa huduma kwa ufanisi pamoja na kuhakikisha wale wanaopokea huduma wanapata huduma bora na salama

Naye Bw. Johansen Kahatano, Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara kutoka LATRA amewasihi wadau hao kutoa maoni kwa ajili ya kuboresha rasimu za Kanuni hizo na pia amesisitiza kwa wale ambao hawakufanikiwa kufika, wawasilishe maoni kwa maandishi kupitia baruapepe ya group.maoni@latra.go.tz mpaka tarehe 26 Mei, 2023.

Kwa upande wake Bw. Richard Toyota, Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya Ziwa (TIRA) amesema ameipongexa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) pamoja naushirikishwaji wa wadau katika kuandaa kanuni ni jambo muhimu na ni sehemu ya utawala bora.

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo