Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

PROF. MBARAWA: KAMILISHENI TARATIBU ZA SAFARI ZA USIKU
Imewekwa: 09 Sep, 2023
PROF. MBARAWA: KAMILISHENI TARATIBU ZA SAFARI ZA USIKU

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb) amewataka wataalamu wa Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kukamilisha kwa haraka rasimu ya utaratibu wa safari za usiku ili Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) wapatiwe maelekezo ya kuanza kutoa ratiba za safari hizo.

Mhe. Prof. Mbarawa amesema hayo Septemba 9, 2023 katika Kituo cha Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS) alipokuwa akizungumza mbele ya Mhe. Selemani Moshi Kakoso (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo ambao wamefanya ziara ya kujifunza kuhusu jinsi LATRA inavyotekeleza majukumu yake.

Aidha, Prof. Mbarawa amesema kuwa, pamoja na Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutakiwa kuweka utaratibu utakaotumika katika kuruhusu ratiba za safari za usiku, ni muhimu kushirikisha wadau katika kufikia maamuzi ya utoaji wa ratiba hizo chini ya udhibiti wa LATRA.

Mhe. Prof. Mbarawa ameongeza kuwa, “Wakati huu ambao wataalamu wanaendelea kukamilisha taratibu hizo, LATRA na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri ikiwa pamoja na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) kuona uwezekano wa safari hizo kwa kuchagua njia zilizo salama na ili pengine safari zianze baina ya saa 1:00 usiku na saa 3:00 usiku.”

Ikumbukwe kuwa, Agosti 8, 2023 LATRA ilitoa rai kwa wamiliki wa mabasi ya masafa marefu nchini wenye nia ya kutoa huduma za usafiri kwa saa 24 kuwasilisha maombi yao ili muda wa kuanza safari hizo utakapoanza rasmi iwe rahisi kufahamu mahitaji halisi ikiwa ni pamoja na maeneo yanayotakiwa kupatiwa huduma hiyo.

Hatua hiyo ni katika kutekeleza agizo alilolitoa Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Juni 28, 2023 kuhusu kuanza kwa safari za usiku kwa mabasi ya masafa marefu nchini.

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo