Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

WASAFIRISHAJI WAASWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKA
Imewekwa: 15 Feb, 2023
WASAFIRISHAJI WAASWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKA

Na Mambwana Jumbe

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri (LATRA) imewaasa wasafirishaji kuungana na kuwa na ushirika wa pamoja ili kuondoa ushindaji usio na tija na kuweza kuongeza kipato chao.

Hayo yameelezwa na Meneja Mradi wa Tiketi Mtandao kutoka LATRA CPA Tadei mwita kwenye semina ya utekelezaji wa Mfumo wa Tiketi Mtandao iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kutolewa kwa wamiliki wa mabasi mkoani Tanga Februari 14, 2023.

CPA Mwita amesema, “kuna tatizo kubwa la ushindani hasi kwa wasafirishaji, wanatoa mabasi mengi kwa wakati mmoja na baadhi ya mabasi yanaenda yakiwa na upungufu wa abiria hivyo inawasababishia hasara kwao, kwa hiyo Mamlaka imekuja na mpango wa wasafirishaji watengeze ushirika kama kampuni na Mamlaka itatoa leseni kwa kampuni au ushirika na hii italeta ufanisi kwa Mamlaka na tija kwa wasafirishaji.”

Naye Bw. Mabula Sambayoka, Meneja wa EFD kutoka TRA amesema wamewaelimisha wasafirishaji kuhusu matumizi ya Mfumo wa Tiketi Mtandao na jinsi ya kuunganisha mfumo huo pamoja na mfumo wa ulipaji kodi ya mapato ili waweze kutimiza takwa la kisheria la ulipaji wa kodi ya mapato Tanzania.

Kwa upande wake Bw. Abdi Awadhi ambaye ni mwenyekiti wa wamiliki wa mabasi mkoani Tanga amesema “tunawashukuru LATRA na TRA kwa kutupatia elimu hii na tunaahidi kuendelea kutumia mfumo huu kwa kuwa una manufaa kwa wote  na tunaahidi kuzifuata kanuni za usafirishaji kama ambavyo tumeelekezwa na LATRA. ”

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo