Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

WASAFIRISHAJI WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
Imewekwa: 12 Feb, 2023
WASAFIRISHAJI WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

Na Mambwana Jumbe

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani  imetoa elimu kuhusu namna bora ya kudhibiti ajali za bararani kwa madereva wa abiria na mizigo ili kuweza kupunguza vifo pamoja na athari zitokanazo na ajali za barabarani.  

Akizungumza hivi karibuni, Afisa Mfawidhi LATRA mkoa wa Manyara Bw. Joseph Michael amasema katika kupunguza ajali hapa nchini, Serikali kupitia LATRA inafanya usajili na uthibitishaji wa madereva kwa kuwapima kupitia mtihani lengo ni kuwa na madereva walioiva na wanaofahamu masuala ya udereva ikiwemo la Sheria na alama za barabarani.

 “Ni dhahiri shahiri kuwa madeva wanaothibishwa na Mamlaka wanakuwa ni wenye ujuzi na weledi hivyo tunaamini kupitia uthibitishaji unaofanywa na LATRA itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza na hatimaye kumaliza tatizo hili la ajali ambazo zimekuwa zikighariu maisha ya watanzania wengi,” ameeleza Bw. Michael

Naye Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Babati, ASP. Joseph Makumu amewasihi madereva kutii Sheria za Usalama Barabarani zilizowekwa ili kuepukana na ajali. “Tunawataka madereva watii Sheria, na barabara zetu zinaongea kwa maana zina alama na michoro hivyo zinaelekeza wapi unatakiwa kulipita gari, wapi unatakiwa usimame na wapi unatakiwa uchukue tahadhari".

Aidha Bw. Joseph Michael amewakumbusha wasafirishaji suala la ukataji wa leseni ambazo zitawaruhusu kufanya biashaza za usafirishaji na pia amewasisitiza wasafirishaji kuzingatia masharti ya leseni hizo.

Naye Hussein Shabani mmoja kati ya madereva kutoka Manyara amesema “tunawashukuru sana LATRA kwa ujio wao wa kutuelimisha, na pia nawashauri madereva wenzangu tuzingatie Sheria za Usalama barabarani kwasababu sisi tunabeba dhamana ya maisha ya abiria tunaowapakia kwenye vyombo tunavyoviendesha “

 

 

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo