Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

HOTUBA YA WAZIRI WA UCHUKUZI MHESHIMIWA PROF. MAKAME MNYAA MBARAWA (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2025/26
15 May, 2025 Pakua

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, tarehe 01 Agosti, 2024 wakati akizindua rasmi huduma ya usafiri wa treni ya kisasa ya abiria kati ya Dar es Salaam na Dodoma Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alielekeza Wizara ya Uchukuzi kuona namna bora ya kuwezesha upatikanaji wa huduma ya tiketi za abiria kupitia dirisha moja. Katika kutekeleza maelekezo hayo, Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Shirika la Reli Tanzania (TRC) na wadau wengine iliratibu na kusimamia mchakato wa kujenga dirisha moja la utoaji wa huduma za tiketi za abiria kwa wasafiri wa mabasi ya masafa marefu na wasafiri wa treni za reli ya kisasa (SGR) na reli ya kati (MGR). Kazi hii imeendelea kutekelezwa na kwa sasa dirisha hilo lipo katika hatua za mwisho za kuanza kufanya kazi na inatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2025.

Pakua taarifa kamili

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo