Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Uchukuzi

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini

Piga Bure : 0800110019/0800110020
LATRA Logo

Karibu

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ni Mamlaka ya Serikali iliyoanzishwa na Sheria ya Bunge Na. 3 ya mwaka 2019, Sheria hii ilifuta Sheria ya Mdhibiti wa awali, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA). Mamlaka imejizatiti kusimamia sekta ya usafiri wa ardhini, hasa usafirishaji wa mizigo na abiria (mabasi ya mjini, mabasi ya njia ndefu, magari ya mizigo, teksi, pikipiki za magurudumu mawili na pikipiki za magurudumu matatu), usafiri wa Reli na usafiri wa Waya.  LATRA ina Makao yake Makuu Dodoma na ina ofisi katika Mikoa yote 26, Tanzania Bara.

Usafirishaji ni huduma ya msingi na kipimo muhimu cha kiwango cha maendeleo katika jamii yoyote. Maendeleo katika usafirishaji huakisi mabadiliko ya namna ya kuishi, ustaarabu na maendeleo ya uchumi.

Katika zama hizi, matumizi ya teknolojia iliyoboreshwa hubadili kabisa sekta mbalimbali ikiwemo usafiri, LATRA inawezesha matumizi ya teknolojia hizo kama ufumbuzi wa changamoto katika sekta ya usafiri. LATRA inafanikisha hayo kwa kuwashirikisha wadau, na wabia wa umma na binafsi. Miongoni mwa mafanikio makubwa ya teknolojia hizi ni Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS). Mfumo huu umekuwa unatumika tangu mwaka 2017 na umeleta mafanikio makubwa katika kuokoa maisha na mali. LATRA itaendelea kuchochea matumizi ya teknolojia kushughulikia changamoto za usafirishaji.

Tovuti hii, imetayarishwa kutoa taarifa, mwongozo na majibu kwa masuala yanayohusiana na LATRA. Pia unaweza kujiunga na Mitandao yetu ya Kijamii, ambapo wadau wetu wanaweza kuwasiliana vizuri na LATRA. Kujiunga na mitandao hiyo, tafadhali tumia kiungo kilichopo chini ya ukurasa huu.

Nawakaribisha wote mtumie tovuti hii kuwasiliana na LATRA.

CPA Habibu Suluo

Mrejesho

Mrejesho, Malalamiko au Wazo