Mheshimiwa Mgeni Rasmi,
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujaalia uhai, afya njema na fursa ya kukutana tena leo kwenye hafla hii ya kukabidhi Cheti cha Uwakala wa Kutoa Leseni za Usafirishaji kwa niaba ya LATRA kwa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Maafisa Usafirishaji wa Pikipiki mkoa wa Dar es salaam (MAUPIDA SACCOS LTD).
Pili, kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi - LATRA, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), natoa shukrani za dhati kabisa kwako wewe Mhe. Albert John Chalamila, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam kwa kukubali mwaliko wetu wa kuwa Mgeni Rasmi na kuja kuhudhuria hafla hii na kuwakabidhi Cheti cha Uwakala wa LATRA kwa Chama Cha Kuweka na Kukopa cha Maafisa Usafirishaji kwa Pikipiki Mkoa wa Dar es Salaam (MAUPIDA SACCOS LTD).